Social Icons


DONDOO MUHIMU KATIKA UCHAGUZI WA VIWANJA:

Ujenzi zone imelenga zaidi katika kupeana uzoefu kuhusu ujenzi wa makazi.Leo tutaongelea dondoo muhimu za kuzingatia katika uchaguzi wa maeneo ili kufikia azma ya ujenzi ulio bora na wa kisasa.

1. Zingatia uchaguzi eneo linaloweza kufikika vizuri,uwepo wa barabara utarahisisha matirio muhimu kama mchanga,matofali,n.k kufika vizuri.

2.Zingatia uchaguzi eneo lisilo mabondeni,na lililo mbali na mto,mfereji,au mkondo wa maji kuepuka usumbufu nyakati za mvua kubwa.

3.Zingatia uchaguzi sehemu ya makazi na isiwe kwenye  maeneo ya viwanda kuepukana na athari za moshi,kelele, hewa zenye sumu na yote yatokanayo, kuepukana na athari za afya.

4.Zingatia  uchaguzi  eneo au kiwanja kinachosimamiwa na mamlaka sahihi za nchi kwa kufuata taratibu, kuepukana na utapeli unaokithiri siku hadi siku.

5.Zingatia uchaguzi eneo lenye upatikanaji wa huduma muhimu kama maji,usafiri,shule,maduka,masoko n.k

6.Zingatia uchaguzi eneo lenye ujirani mzuri na nyumba za makazi,kusiwe na vilabu vya pombe,makumbi ya starehe,n.k ili kuboresha malezi mema kwa jamii.



No comments :