Social Icons


HESHIMA KWA FUNDI PAA

Paa ni moja kati ya vigezo muhimu katika kukamilisha ujenzi wa makazi yaliyo bora.Hakuna nyumba bila paa,umuhimu wake unafahamika dhahiri kwa kila mmoja wetu. Kuna paa za aina mbalimbali,leo nitaongelea paa lililozoeleka kwa miaka mingi nchini kwetu Tanzania.Haihitaji pesa nyingi kupendezesha nyumba kwa bati la gharama kubwa kuzidi uwezo wa mwenye nyumba,kama ambavyo wengi wamekuwa wakifikiri kwa miaka ya sasa.                        
kwa mtazamo wangu tunahitaji fundi mzuri anayeweza kulitendea haki paa kuanzia uezekaji wa mbao (kenchi)mpaka kufunika.Nina imani na mafundi wazoefu wa kitanzania wanaweza kutoa kazi nzuri kama hizi.
Bati hili limezoeleka sana nchini kwetu na bado linafanya vizuri,na zaidi wengine hupenda kupaka rangi iwe bluu,maruni,nyekundu,kijani na bado linaongoza kwa gharama nafuu kulinganisha na mengine.

Heshima kwa baba mwenye nyumba,heshima kwa bati letu,heshima kwa fundi paa.(picha kwa hisani ya wadau wa ujenzi zone)

No comments :