Social Icons


KITCHEN IDEAS

Ujenzi wa kisasa unajumuisha uwepo wa jiko la ndani lenye kujengewa makabati yenye kuhimili ubebaji wa jiko liwe la gesi au umeme,wengine huweka sehemu ya partition kwajili ya microwave  na zaidi sink lenye bomba za kutolea maji kwajili  ya kuoshea vyombo ni muhimu  sana.Ujengaji wa tiles  katika eneo la jiko nao ni sehemu muhimu katika kukamilisha unadhifu na muonekano mzuri wa jiko sababu ni rahisi kuzisafisha muda wowote kwa urahisi.katika zile kabati za majiko haya wengi hupendelea kujengea mawe yaliyochongwa vizuri hasa marble au granite na hii hutokana na chaguo na uwezo wa muhusika,wengine hujengea makabati kwa cement na tofali na juu wanakava kwa tiles,yote ni chaguo na uwezo wa mwenye nyumba.Mbao za aina mbalimbali zilizo ngumu hufanikisha vyema ujenzi huu wa kitchen cabinets mfano mninga au mkongo,sababu znahimili na kudumu muda mrefu.Wengine hupendelea mbao aina ya marine boards nazo hutoa kazi nzuri na znadumu japo sio rafiki sana na maji,pia ukitumia marine boards inapendeza ukizipaka rangi kwa ule utaalam wa kuspray kwa compressor.Wengine hutumia mdf nazo hutoa kazi nzuri japo zote zinahitaji uangalifu wa kina hasa kuzikinga na maji.kama ilivyo ada yetu tunakupa ideas kwa mifano ya picha "kazi ya kwanza  namba za fundi ni(0719 136699).

NOTE:HATUBEBI DHAMANA YA KAZI ZITAKAZOFANYWA NA MATANGAZO HAYA.

No comments :