Habari za leo mdau wangu wa ujenzi zone blog.leo nitashea uzoefu wangu kuhusu ujenzi wa nyumba zetu za makazi.
Wengi wamekuwa na hofu kuwa ukitaka kuanza ujenzi unatakiwa kuwa na mapesa mengi,hii hutokea pale wanaposikia kwa wenzao waliojenga kuwa nyumba zao zina thaman ya sh milion 150,basi hufikiri kuwa mpaka uzishike mkononi cash ndio uanze ujenzi'lahasha sio kweli japo ukiwa nazo cash sio vibaya.
Dondoo muhimu katika kufanikisha mipango ya ujenzi wako ni hizi zifuatazo...
1. Muhimu ni kuwa na nia kabla ya kitu chochote.
2.Baada ya kuwa na nia unapaswa kuwa na namna ya kujipatia kipato kwa njia zilizo halali ili uweze kujinunulia ardhi ya kufanikisha ujenzi wako.
3.Jitahidi uwe na plann kichwani mwako juu ya nyumba unayoitamani kuishi ndani yake miaka ijayo.
4.Ukishakuwa na ramani kichwani sasa waweza tafuta wachoraji wataalamu mkashirikishana juu ya kile unachokitamani,na pia kama una picha ya nyumba,au plann waweza mpatia mkaifanyia marekebisho ili upate unachokitaka.
5.Baada ya kuwa na ramani ni vizuri ukampata mtaalamu wa makadirio akupe BOQ( bill of quantity) ikusaidie kujua unahitaji matirio za aina na za gharama gani ili kufanikisha ujenzi wako.
6.Baada ya kuwa na hivyo vitu muhimu ni vyema ukampata fundi mtaalamu na mzoefuu zaidi akatizame eneo lako na ramani yako ili mshauriane jinsi ya kuanza ujenzi na gharama za ufundi.
7.Ikumbukwe kuwa hizi procedure zinafanyika kwa vipindi tofauti kadiri ya uwezo wako kifedha sababu kuwa na hao wataalamu kunahitaji fedha za malipo.
8.Sasa umeshajua gharama na una picha kamili ya vitu unavyohitaji kukamilisha ujenzi wako,Unaweza kuingia kwenye utaratibu wa manunuzi ya vitu muhimu visivyoharibika.
8.Kabla ya manunuzi ni vyema ukaandaa stoo na mlinzi atakayekulindia eneo lako na vifaa.(wengine hujenga vyumba vya mabati).
9.Uwezo ukiruhusu waweza anza andaa kisima cha kuhifadhia maji au tank sababu maji ni muhimu mno,pia waweza nunua matofali,mchanga,kokoto,nondo,mawe,mbao.(cement ikihifadhiwa vbaya huganda hivyo haishauriwi uinunue kabla,labda uilipie dukani kwa muuzaji wa jumla unayemuamini)
10.Taratibu waweza anza ujenzi wa msingi na mwishoni ukafika mbali mpaka kupaua ukienda kwa hatua hizo kadiri ya kipato chako.
NOTE:HATUA HIZI ZAWEZA KWENDA TARATIBU KADIRI YA KIPATO CHAKO AU HARAKA KADIRI YA MIPANGO YAKO YA FEDHA' NAWAASA WENGI WASIOPITIA KWA WATAALAMU WAANZE SASA ILI KUEPUSHA HASARA ZA HUKO MBELENI.
KUJENGA NI MIPANGO (TIPS MUHIMU KUFANIKISHA UJENZI)
Labels:
UJENZI WA MAKAZI
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
3 comments :
Asante Jaq kwa kututia moyo,na tips hizi nzuri.
MDAU....naweza pata ramani ya nyumba hii...0688 555578.
asante sana.
mike.
asante sana kwa elimu yako ya matumaini!..hii nyumba hapo juu ni ya vyumba vingapi!
Post a Comment