Social Icons


KITCHEN IDEAS KWA NYUMBA ZENYE SIZE NDOGO

Matumizi ya mbao aina ya mkongo,mninga n.k yameongeza upatikanaji wa fenicha mbalimbali zenye uimara na mvuto pale zinaponafanyiwa finishing nzuri ya msasa na vanish  hata na rangi.
Leo ujenzi zone itashea nanyi majiko yanayofaa kwa nyumba za size ya kati hususani majiko yenye makabati ya mbao.
Uimara na umaridadi ndio sifa kuu ya mbao hizi.
Kwa nyumba kuwa ya kisasa inapendeza zaidi kujengea jiko la ndani hata kwa kutumia kuta moja kama baadhi ya picha zinavyoonyesha.
Kikubwa ni kuwa huhitaji nyumba kubwa saana kuweza kumiliki jiko la ndani,hata wenye nyumba za size ndogo wanaweza pata ideas za kujenga majiko ya kisasa kwa nyumba zao.
(Picha nne za mwisho ni kazi ya fundi huyu,Fundi makabati 0719136699.)

RANGI ZA NJE YA NYUMBA ZINAZOROCK

Hii ni moja kati ya rangi zinazofanya vizuri zikipakwa nje ya nyumba.Rangi hii huchanganywa kwa teknolojia ya compyuta kwa maduka yanayohusika na rangi.mvuto huzidi ikichanganywa na nyeupe katika baadhi ya sehemu kama inavyoonekana pichani.

KITCHEN ORGANIZER IDEAS

SHOWER CABIN FOR SALE

Mdau anauza hizo bafu za kisasa kwa bei nzuri.Alizinunua akazifunga kwake ila hajawah kuzitumia na nyumba haijahamiwa.hiyo ya kijani ni shilingi laki 5 na hiyo nyeusi ni shilingi milioni 1.ukihitaji nipigie 0786808707

WASHROOMS DESIGNS

Ujenzi zone leo itashea nanyi washroom za kisasa.Muhimu ni kuwa hakuna asiye na matumizi na vyumba hivi hivyo usafi wa mazingira yake muda wote ndio hukamilisha muonekano mzuri.
Zipo aina nyingi sana za mabafu ila kwa wote hazitakosa vitu muhimu kama tiles,toilet sink,na washing basin pamoja na shower cabin za kuogea.Inahitaji uchaguzi sahihi wa vifaa hivi ili vidumu na kufanya kazi vzuri.Muhimu ni utunzaji mzuri na kuweza kuvimaintain pindi vinapoleta hitilafu ndogondogo.Uwepo wa makabati kwajili ya uhifadhi wa vitu mfano mataulo,sabun,dawa za kusafishia n.k nao
Tiles au glass bloks ndio hufanikisha mvuto wa vyoo vyetu.wengine huweka ukuta mzima wengine huweka nusu ila vyovyote iwavyo tiles hutunza unadhifu wa washrooms zetu.Pichani utajionea ideas mbalimbali za washroom za kisasa.

BEFORE AND AFTER YA MDAU WA UZ

Pongezi nyingi Zikufikie mdau wangu kwa kuthubutu jambo la msingi kama hili.Kifupi ni kuwa mdau alikuwa na kiwanja tu bila nyumba..Sikumoja aliona post inayohamasisha wanawake wajenge na wapunguze kuconcetrate na mapambo yenye gharama sawa na vifaa vya ujenzi mfano handbag laki na nusu ni tofali 150,lesswigg laki tatu ni mifuko ya cement 20,simu kali za smartphone n.k Alifanya maamuzi tangu sikuhiyo kuanza ujenzi kwa kidogo alichonacho na mpaka sasa ametumia miezi 11 kufikia hapo japo hapo katikati alikuwa anasimama kidogo.
Mdau ameishukuru group ya Ujenzi zone facebook kumuhamasisha kuanza ujenzi na pia amemshukuru aliyepost kuhusu wanawake na ujenzi.HONGERA NYINGI KWAKO MDAU NA TUNATEGEMEA SOON KUPOKEA PICHA ZA FINISHING.

UBUNIFU WA VIUNGA VYA MAUA NA MATUNDA MAJUMBANI KWETU.

Watu wengi wamekuwa na nyumba nzuri na za kuvutia hata wengine kutamani kuchukua Ramani hizo za nyumba na wao kujenga kama hizo, uzuri wa nyumba hizo Mara nyingi huchangiwa na mambo mengi sana ikiwemo na Mwonekano mzuri wa Viunga na mpangilio mzuri ndani na nje ya ukuta kwa kuweka maua Mazuri yanayovutia pia Baadhi ya Matunda kama yanakubari katika eneo hilo. Hizi ni Baadhi ya Picha ambazo zinaonesha Mwonekano wa viunga ndani ya nyumba moja katika maeneo tofauti tofauti.
Tunakaribisha Maoni kwa wanaujenzi Zone.

Picha na Ujenzi Zone.

METAL FENICHA KWA GHARAMA NAFUU.

Ujenzi zone inakaribisha oda za madirisha,milango,mageti,viranda na vitu vyote vinavyotengenezwa kwa chuma.
Tunakupimia  madirisha yako na kukupa picha uchague sampo au ufike workshop kuchagua sampo zetu,kisha tunakupatia quotation ukiridhia kazi inaanza kwa advance,mwishoni tunakusafirishia,tunakufitishia kwa gharama nafuu.0786808707wahi sasa na ofisi iko goba tatedo watsap 0717060776

NYUMBA KALI ZINAZOROCK UJENZI ZONE

Inapendeza na kutia moyo kuona mwamko wa wadau kuhusu habari zihusuzo ujenzi especially kwenye mitandao yetu ya kijamii.Ujenzi zone group iliyopo facebook na sasa kwa blog imekuwa ikishea ideas mbalimbali kuhusu ujenzi wa nyumba za kisasa.Kuona picha na habari hizi kila siku kwa wengine hakutakuacha bure bila mwamko fulani na mawazo tofauti utaipendezeshaje nyumba yako,kwa waliokwisha kujenga,halikadhalika wanaoanza ujenzi.SEGMENT HII YA NYUMBA ZINAZOROCK UJENZI ZONE IPO VERY POSITIVE NA SIO KWA MAANA NYINGINE..NAKARIBISHA PICHA NA MAONI MBALIMBALI KWA WATSAP NAMBA 0717060776(SHUKRANI ZA PEKEE KWA MDAU WA UJENZI ZONE KUSHEA NASI PICHA ZA NYUMBA YAKE YA KISASA,HONGERA SANA)

GHOROFA ZA KISASA

Ni ndoto za walio wengi kumiliki nyumba za kisasa,zaidi ni ndoto za hakika kuwa wengi wetu hutamani kumiliki maghorofa.
Kwa mtanzania wa kawaida kumiliki ghorofa ni mafanikio na haitapotea dhana ya kuwa ghorofa ni nyumba za wenye uwezo zaidi na hii ina ukweli ndani yake kutokana na gharama za ziada zinazojitokeza kwenye ujenzi wake tofauti na nyumba za kawaida.
Ujenzi wa ghorofa za kisasa huzingatia uwepo wa mtaalamu na mzoefu kuweza kusoma ramani husika na kusimamia ujenzi.
Vifaa hutumika vya ziada kiutaalamu zaidi  mfano nondo,mbao,cement na tofali wengi hupendelea inchi 6na huzilaza kuongeza uimara wa kuta kuhimili mzigo wa juu.
Inapendeza kuwa na eneo kubwa na kutosheleza kwa mazingira ya nje kuweka bustani nzuri za maua na ukoka.
Ghorofa hubeba vyote vinavyofanyika kwa nyumba za kawaida ila vinatumia utaalamu wa tofauti kiasi mfano wiring,plumbing..
Ghorofa huvutia ikiwa na balcony na madirisha makubwa ya kutosheleza na zaidi hupendeza kukiwapo na pergola kama inavyoonekana pichani(paa ya mbao katika baraza /balcon).
Zipo ghorofa za aina nyingi ila leo tunaongelea ghorofa za makazi,maranyingi hazizidi floor 2,na hujitosheleza vyumba vya kawaida na vile vya ziada.
(kama ilivyo ada tunakamilisha somo kwa picha makini).
Enjoy...

GEBO STYLE STILL ROCKS..

Uezekaji wa nyumba upo wa aina nyingi,kuna wanaofikia stage ya linta na kujengea tofali course mbili au tatu kisha wakafunga kenchi na kuweka bati,kuna wanaofikia linta kisha wakamimina jamvi kwa juu mfano wa gorofa inayoendelezwa juu na kuifanyia finishing nzuri.
Leo tutaangalia style ya kujengea tofali kwenda juu kutengeneza shepu mfano wa v iliyoinama almaarufu kwa jina la gebo.Dizain hii imetumika sana hapo zamani  kwa nyumba aina zote hasa magorofa na bado inatumika kwa wale wenye kuipenda na kuifurahia.Miaka ya sasa wengi hupendelea style ya kutengeneza gebo kwa kenchi ila hii ilitegemea zaidi tofali kuleta muonekano mzuri wa paa.kama ilivyo desturi ujenzi zone inakupa somo kwa picha makini na hakika utafurahia na kuielewa gebo kwa ufasaha.(Picha ya mwisho ni kutoka kwa mdau wetu wa ujenzi zone hongera sana kwa nyumba yenye mvuto.)