Social Icons


GHOROFA ZA KISASA

Ni ndoto za walio wengi kumiliki nyumba za kisasa,zaidi ni ndoto za hakika kuwa wengi wetu hutamani kumiliki maghorofa.
Kwa mtanzania wa kawaida kumiliki ghorofa ni mafanikio na haitapotea dhana ya kuwa ghorofa ni nyumba za wenye uwezo zaidi na hii ina ukweli ndani yake kutokana na gharama za ziada zinazojitokeza kwenye ujenzi wake tofauti na nyumba za kawaida.
Ujenzi wa ghorofa za kisasa huzingatia uwepo wa mtaalamu na mzoefu kuweza kusoma ramani husika na kusimamia ujenzi.
Vifaa hutumika vya ziada kiutaalamu zaidi  mfano nondo,mbao,cement na tofali wengi hupendelea inchi 6na huzilaza kuongeza uimara wa kuta kuhimili mzigo wa juu.
Inapendeza kuwa na eneo kubwa na kutosheleza kwa mazingira ya nje kuweka bustani nzuri za maua na ukoka.
Ghorofa hubeba vyote vinavyofanyika kwa nyumba za kawaida ila vinatumia utaalamu wa tofauti kiasi mfano wiring,plumbing..
Ghorofa huvutia ikiwa na balcony na madirisha makubwa ya kutosheleza na zaidi hupendeza kukiwapo na pergola kama inavyoonekana pichani(paa ya mbao katika baraza /balcon).
Zipo ghorofa za aina nyingi ila leo tunaongelea ghorofa za makazi,maranyingi hazizidi floor 2,na hujitosheleza vyumba vya kawaida na vile vya ziada.
(kama ilivyo ada tunakamilisha somo kwa picha makini).
Enjoy...

1 comment :

Anonymous said...

welcome to www.fun-tz.blogspot.com