Social Icons


BIG SPACE NDIO HABARI YA MUJINI..

Wadau leo tutajionea ujenZi  wa makazi bora katika viwanja vyenye nafasi kubwa.Kutokana na kukua kwa miji yetu nafasi za ujenzi zimekuwa adimu kiasi kwamba hata nyumba zetu zinakuwa na uhaba wa nafasi nje na ndani.
Hii ni kutoka kwa mdau wetu anayeishi Zambia,tunamshukuru kushea nasi nyumba yake na sehem muhimu za nyumba.
Pale nafasi inaporuhusu kumiliki eneo kubwa inapendeza mno kujenga nyumba kubwa yenye nafasi ya kutosha kama alivyofanikisha mdau wetu leo.Nyumba yake ni kubwa na ina nafasi nje na ndani kama inavyoonekana pichani.
Nafasi ya korido ndio iliyonigusa zaidi,mzunguko wa hewa ni mkubwa kila sehemu hata parking imejitosheleza.
Hongera mingi mingi kwa mdau hakika nyumba yako ni nzuri inavutia na umezingatia maboresho ya afya, kuishi kwenye nyumba  yenye mzunguko wa  hewa ya kutosha.
Nanyi wadau wangu wa Ujenzi zone msisite kuiga mfano huu pale uwezo unaporuhusu...Nyumba bora  ni nafasi...

No comments :