Social Icons


DONDOO MUHIMU KABLA YA KUANZA UJENZI

Habari zenu wadau wa ujenzi. Natumaini mko na afya njema na mnaendelea vyema na majukumu ya kulijenga taifa. Kama ilivyo ada blog yetu ya ujenzi zone tunashea uzoefu wa mambo mbalimbali yahusuyo ujenzi.
Ieleweke wazi kuwa mada mbalimbali zinazoongelewa hapa ni kutokana na uzoefu wa maisha halisi ya mtanzania.

Tulishaongelea dondoo muhimu za kuzingatia wakati wa kutafuta viwanja au maeneo ya kujenga.
leo tutagusia zaidi kwenye vigezo vya kuzingatia kabla ya kuanza ujenzi.

1. Maandalizi ya eneo husika kwa kusafisha iwapo kuna pori,vichaka au majani,na miti.
2. Muhimu uandae stoo ya kuhifadhia vifaa vyako vya ujenzi pamoja na matirio muhimu kama cement,nondo n.k wengine hujenga stoo au kuhifadhi kwa jirani.
3.Barabara ya kufikisha matirio kama mchanga,tofali n.k ni muhimu iwe katika hali nzuri hadi ilipo site yako,itasaidia matirio zisishushiwe njiani ukaingia extra cost kuzisogeza site.
4. Zingatia uwepo wa toilet ndogo ya dharura kuweza kuwasitiri mafundi kipindi cha ujenzi.mfano wengine huanza na shimo la soak  away pit litakalokuja tumika hapo baadaye kwa kujengea toilet juu yake.
5.maji ni muhimu yawe na storage tank kubwa kama kisima cha chini,tanks kubwa au caro la kujengwa juu, ikumbukwe uimara wa nyumba hasa mwanzoni unaposimamisha jengo kabla ya finishing hutegemea maji.
6. Upandaji wa miti ya vivuli kama eneo halina miti ya maua huanza mwanzoni wa ujenzi kutegemeana na chaguo la mwenye nyumba.
7.Zingatia ununuzi wa vitu kama ngazi,wheelbarow,pipa/ tank,mpira wa kumwagilizia maji,n.k kwa matumizi ya site.mara nyingi hivi ni nje ya vifaa vya ufundi atakavyokuja navyo fundi mjenzi.

NOTE: Dondoo hizi ni muhimu kwa mwenye nyumba anayeanza ujenzi kuzingatia.Waweza ongeza nyingine mdau wa ujenzi kadiri ya uzoefu wako..

No comments :