Social Icons


WASHROOM IDEAS(BLACK AND WHITE TILES ROCKS)

Nyumba bora ni pamoja na uwepo wa bafu na choo cha kisasa,kadiri miaka inavyosogea na ubunifu wa vitu hivi unatokea zaid na zaidi.kuna mabafu ya kusimama na hata ya kukaa kadiri ya chaguo lako.
Jenga ujengavyo,ila kama haujajenga choo(toilet)ni kazi bure.Starehe ya mwanadamu iko pale!Yatupasa kujenga system nzuri na imara za utoaji maji taka,halikadhalika vyumba vya  kuogea  na chumba kitakachowekwa toilet sink vinafaa viwe vikubwa na madirisha yawe makubwa kuruhusu mzunguko wa hewa.matumizi ya tiles iwe ukuta wote au nusu ukuta na chini kwa floor vimeboresha utunzaji wa mazingira ya vyoo vyetu na mabafu.
Usafi wa vyoo na mabafu ni muhimu uzingatie kila dakika aingiapo mtu kupatumia akimaliza asafishe ili mwingine au yeye mwenyewe akirudi akute pako safi.
Leo nafurahi kushea nanyi toilet ya mdau wangu,ameweka tiles nzuri black and white chini na ukutani na hakika panavutia na pasafi.hii sio google, wadau wanafanya kweli hakika watanzania tunaweza.zaidi utaona picha ya bafu la kisasa haihitaji kuyasukuma maji kwa fagio wala brashi,zinaitwa shower cabin kwa lugha za wenzetu.mwishoni utaona mabafu ya wenzetu(tiles nyeusi zinafaa bafuni) na mwishoni utaona bafu la crazy colour.

No comments :