Social Icons


FROM NOTHING TO SOMETHING...

Safari hii ni ndefu sana na bila shaka ina headache za hali ya juu ambazo huwa hazihesabiwi kabisa katika utaratibu wowote wa gharama ya nyumba.
Ifike pahala tuwaheshimu wenye nyumba na kuzijali nyumba zao katika mazingira yoyote tunayojikuta tunaishi katika nyumba hizo.Uwe ni mpangaji,au mfanyakazi bado unawajibishwa kutunza nyumba hizi ili zidumu zaidi.
Imekuwa ni desturi kuona baba mwenye nyumba au mama mwenye nyumba ni mkorofi na adui ila utakapojikuta umeanza safari hii ndio utagundua kwanini na wao walipanga masharti mengi na hata walikereka kuona mwanao anapochora ukuta na mkaa au na msumari.
Muhimu ni kuwa tuheshimu, tutunze,na tuthamini jitihada za wenye nyumba kwani safari hii sio pesa tu ndio huiongoza bali muda na kujitoa kwa hali juu tena kwa wenye hofu ya mungu tunasema safari hii ni kwa neema zake mungu ndio huifanikisha.
Nawatakia safari njema mnaoanza ujenzi,mlio hatua za katikati,na mliomaliza nawapongeza sana munayo haki  ya kuzisimamia nyumba zenu kwa umakini wa hali ya juu ili zizidi kudumu.
HESHIMA KWA BABA NA MAMA MWENYE NYUMBA.Mujini wanasema hakuna baba  mwenye gari ni baba mwenye nyumba tuu.(shukrani kwa wadau wote wa ujenzi zone kufanikisha uwepo wa picha hizi)

1 comment :

Unknown said...

Naomba namba ya simu ya fundi aliyetengeneza skating ya picha ya nane.