Social Icons


SITTING ROOMS ZINAZOROCK...

Blog yako ya Ujenzi zone leo itakupa somo kuhusu mionekano tofauti ya sebule zetu zinavyotakiwa kuwa' na hii yote ni kukuongezea ideas ambazo ukizifanyia kazi utaifanya sebule yako iwe paradiso ndogo na kukuvuta uwahi nyumbani muda wote.
Muhimu kabisa kwa tunaoanza ujenzi tuzingatie kuzipa sebule zetu nafasi ya upendeleo ili ziwe na hewa na mwanga wa kutosha kuhimili mzunguko wa watu.
Pili,tuzingatie urembo wa ceiling kama gypsum basi iwe na muundo tofauti kidogo na vyumbani ilimradi mvuto uongezeke.
Wakati ujenzi unaendelea waweza dizain nguzo fulani au steps za kushuka au kupanda plus tv wall ilimradi pawe na mvuto wa kile unachokipendelea,wengine hujengea glass blocks kwa ndani,pia kabati la kuweka tv ni vyema likadzainiwa likae wapi mapema(showcase).
Baada ya ujenzi zingatia taa nzuri,rangi tofauti kwa ukuta mmoja, picha nzuri za ukutani,shelves za kisasa nazo huongeza umaridadi,makochi mazuri,capet nzuri na coffee table nzuri.
Hauhitaji makorokoro mengi sana kuipendezesha sebule yako ni kuwa na usefull staffs chache na zenye muonekano mzuri.
Wall pepa zikidizainiwa vizuri especially kwa kuta moja mfano tv wall nazo huvutia sana.
Picha za ukutani ni vyema ikawa moja kubwa na nzuri na sio zijae kuta pande zote za sebule,nyingine weka kwa corido na kadhalika,maana zikizidi mbili inakuwa sio tulivu.
Jionee kwa picha na utapata wazo..(Specially thanks kwa mdau wetu Abed Gallus Abed kushea nasi  baadhi ya picha za sebule).HAUJACHELEWA KUSHEA NASI PICHA ZA VITU MBALIMBALI VIHUSUVYO UJENZI NA USIACHE KUTANGAZA NASI 0717060776 WATSAP

No comments :