Social Icons


BATHROOMS DECORATION"TIPS MUHIMU..

Nyumba bora  hukamilishwa na maliwato safi..Jenga uwezavyo ila hujaweka bafu na toilet basi bado hujakamilisha ujenzi.Wengi hupenda kumix the two yaani bafu na toilet kutegemeana na matumizi yao especially kwa master bedrums zao.
Umiliki wa mabafu ya kisasa huhusisha vitu muhimu na vyenye kuongeza muonekano fresh wa mabafu yetu.
Ujenzi zone itashea nasi vitu muhimu kukamilisha mabafu ya kisasa yenye mvuto maridhawa kama yanavyoonekana pichani.
1.Space ya kutosha hii ni siri kuu ya kwanza.
2.chaguo la rangi,zingatia zinazoshine ili pasiwe na giza,crazy colours zimefanya vizuri pichani,usisahau taa nzuri juu na hata kwenye vioo.
3.Tiles chini na ukutani haijalishi ni half way au full wall huwa zinaongeza sana muonekano mzuri.
4.Sink ziwe comfortable kutumia hivyo muhimu uzifitishe kwa akili na uzingatie vipimo pale znapowekwa .wakati mwingine pia zijaribishe kabla haujanunua ukipata hiyo chance.
5.Zingatia uimara wa vifaa vyote vya fittings hapa jali ubora ili usiwe na kazi kubadilibadili daily.
6.Usafi ndio pambo namba moja kisha tumia dawa zenye kudumisha usafi na kuua wadudu plus weka vitoa harufu nzuri iwe mawe,spray,au maua vingi hupatikana kwa supermakerts.
7.Usisahau vitu muhimu  japo ni vidogo kukamilisha matumizi sahihi ya mabafu pamoja na muonekano mzuri,carpets,taulo na reli zake, showcase ya maua na perfumes,zaidi toilets cabinets kuhifadhi vitu vya bafuni mfano sabuni na dawa za toilets.
8.....kwa leo ujenzi zone imekupa hizo tips chache ila nyingine ruksa kujiongezea.

No comments :