Wengi tumeshazoea na ni desturi kujenga nyumba zenye eneo la kukutania na kubadili mawazo,wakati wowote iwe asubuhi au mchana.
Sebule ni muhimu sana kwa nyumba zetu na huwa ni sehem ya starehe kwa namna moja ama nyingine.
Muhimu sebule iwe na nafasi kuweza kuingia fenicha za aina mbalimbali,kama makochi,meza na kabati la televisheni.
Pili uchaguzi mzuri wa rangi za ndani nao huweka mvuto maridhawa kwa ndani hapa zingatia rangi zilizopoa.
Tatu dizain ya ceiling nayo ni pambo kwa sebule zetu ukiweka na taa nzuri,za gypsum.
Zingatia uchaguz mzuri wq tiles zinazoendana na rangi za ndani.
Madirisha makubwa nayo huongeza mvuto ukijazia na pazia ndefu zenye curtain rods nzuri,iwe ni chuma au aluminum au mbao.
Zingatia urembo wenye kumech rangi japo kias kidogo na rangi kuu zilizotawala mfano waweza weka vase au picha ya ukutani yenye kuwiana na rangi zilizopo.
Ukimudu kuweka zile shelf za ukutani nazo husaidia frem za picha kuwa dsplayed vizuri.
Wale wanaopendelea wall pepa inapendeza kuziweka kwenye ukuta mmoja hasa inapokaa tv na music system.
Usafi ni pambo kuu kwa sebule zetu na pia tujifunze kupunguza makorokoro na mazagazaga yasiyohusika,mfano magazeti,mavitabu,makasha ya cd,maua ya kila rangi nayo hayapendezi kurundikwa sebuleni.
Ushauri ni kuwa tusijilemaze kusema siwezi kuwa na sebule makin kama zilizopo pichani kisa wanangu wadogo..ikumbukwe watoto hawahawa tunaenda nao mahospitalin,au mahotelini na wanajua kujisitiri na kuheshimu vilivyopo hivyo ni kuwazoesha na kuwajengea umiliki kuwa wao ndio wakuitunza sebule ya nyumbani..
No comments :
Post a Comment