Social Icons


BEDROOM IDEAS...


Ni kweli iliyo dhahiri kuwa vyumba vyetu vya kulala vimetofautiana sana na vya mahotelini.
Imefika pahala tumeanza kuhalalisha kuwa hotelini ndio kunatakiwa kuwe kuzuri na kusafi tena kulikopangika vizuri.
Si kweli tuondoe mawazo hayo kwa kupendezesha vyumba vyetu vya kulala ili navyo viwe vinarock kama vitanda vya 5stars hotel..tuzingatie yafuatayo.
1.Muhimu chumba kiwe na nafasi ya kutosha ili kitanda kikae katikati,au kikae katika hali ya kiweza kukizunguka pande zote ili iwe rahisi kusafisha.
2.Muhimu kuweka vitu vichache vyenye kuendana na hoby yako kama wewe ni wa kusikiliza sana music basi weka redio ndogo,kama wewe ni wa tv weka television..japo wengi hushauri isiwekwe vyumbani ili isivuruge utaratibu wa usingizi.
3.kochi dogo na kapeti dogo linalowekwa pembezoni huleta muonekano mzuri.
4.kabati hazishauriwi sana kwa wale wenye nafasi za kutosha majumbani inapendeza kujenga chumba cha nguo na viatu,ila kwa wale wenye nafas za wastani inapendeza kabati likawepo moja lenye mipangilio mizuri.
5.Taa nzuri zenye muonekano mzuri nazo ni pambo la chumbani,zaidi kuna haja ya kuseti taa za aina mbalimbali,hasa zile za mwanga mkali na mwanga hafifu.
6.Mwisho wa yote ni kuepuka kuweka mazagazaga yasiyotumika haijalishi nyumba ni kubwa au ndogo,na kutandika kitanda muda wote kuwe kusafi na hakika utakifurahia chumba chako.

Maelezo zaidi kwa picha.





No comments :