Social Icons


TIPS MUHIMU ZINAZOHUSU UCHAGUZI WA PAA,TOKA KWA WAKALA WETU MUAMINIFU NASSOR LIPANGILE

SOMA TIP MUHIMU YA KUZINGATIA TOKA KWA MTAALAMU WETU WAKALA WA MABATI  MUAMINIFU Nassor Lipangile.

MDAU ALIULIZA VIGEZO VYA KUJUA BATI IMARA LISILOPAUKA MAPEMA!
JIBU TOKA KWA WAKALA...
Swali zuri sana katika bati kuna vitu viwili vya msingi vinaangaliwa cha kwanza ni unene wa bati (thickness) ambayo hapa kwetu inapimwa kwa kutumia  gauge yaani kuna g32, g30 ,g28 na g26 kadri hizi gauge zinavyokuwa ndogo ndio bati linavyokuwa nene g28 ndio standard kwa hapa Tanzania. G32 ni nyembamba sana na haifai kabisa kutumia g30 watu wanatumia lakini nayo bado sio standard  lakini g28 na g26 ndio bora zaidi kabisa.
Kitu kingine kinaangaliwa ni material iliyotumika kutengeneza kwa hapa nchini kuna bati za aina tatu
1.Galvanized (GI) hii ni chuma kitupu ni rahisi kushika kutu na hazifai kabisa hususan maeneo ya pwani mara nyingi kampuni za kichina ndio wanatengeneza bati hizi.
2.Aluzinc/zinclume(AZ) hizi ni bati za chuma kilicho changanywa na Aluminium ndio bati sahihi zaidi kutumia zina uwezo wa kudumu muda mrefu kwani chuma chake hulindwa na Aluminium kwa hiyo hazishiki kutu wala kupauka kilahisi. Kwa hapa nchini AZ ya uhakika ni kampuni ya Alaf maana nayo inaviwango vyake.
3. Aluminium pure.
Hizi ni bati zilizotengenezwa kwa kutumia Aluminium hazishiki kutu wala kupauka kabisa hapa nchini utazipata kupitia kampuni ya metal products.
Na kigezo cha mwisho ni aina ya rangi iliyotumika kama unahitaji bati za rangi kuna rangi za mimea (organic) ambazo ni bora zaidi huwa hazipati reaction yoyote na kuna rangi za kemikali ambazo zikikutana na hali ya hewa zinafanya reaction na kupauka.
Kwa maelezo zaidi, ushauri kupata hizi bati kirahisi na kwa uhakika karibu dukani kwetu FTN Hardware. Tazara,veternary  mandera rd opp kilimo au wasiliana kupitia 0754259179/0715916836

No comments :