Social Icons


FAHAMU HATUA ZA KUFUATA UNAPOTARAJIA KUJENGA GHOROFA YA MAKAZI

MADA YAHUSU HATUA ZA UJENZI WA NYUMBA ZA GHOROFA ZA MAKAZI..
Mada hii imetokea facebook kwenye group yetu ya ujenzi zone(sikia maoni ya mmoja wa wadau wenzetu)

Kawaida... Taratibu za ujenzi huanzia kwenye wazo Fulani alilo nalo anaetaka kujenga, inawezekana akawa tayari ana plot au bado haijainunua hiyo plot, then humuona architect na kumuelezea wazo lake either kwa maneno , sketch au picha, architect atamshauri kulingana na utaalamu na uzoefu wake kuhusu aina hiyo ya mradi, uwaje ili uwe na tija na ufikie malengo ya mteja, baada ya kupata maelezo, sketch, kuangalia KIWANJA na kufanya survey ya levelling site.. Architect hufanya proposals ya mchoro mpaka client atakaporidhia ndipo mchoro wa mwisho hufanywa, BAADA ya kukamilika mchoro wa usanifu, hatua inayofuata NI kuandaa mchoro wa structural, yaani engineering structural drawings ( unahusisha size ya nondo, idadi ya nondo, aina ya nondo, spacing ya nondo, ukunjaji wa nondo, lap length etc).
N.B mchoro yote inatakiwa iwe NA mihuri ya trusted firm.

BAADA ya hapo hupelekwa keener building council KWA kuidhinishwa..

Ikiidhinishwa unatafuta Quantity surveyor ili akukokotolee gharama za ujenzi . .

Baada ya hapo, hutafutwa mjenzi though mamlaka hutaka kampuni za kikandarasi ndio zijenge ili risk zote za ujenzi zichukuliwe na kampuni, lakini hata fundi mzoefu anaweza kuijenga, ikiwa ni ghorofa chache.

Kuhusu ukubwa wa KIWANJA ni vyema ikaanzia 12×12  baada ya hapo procedure za ujenzi yaani kuhamisha kilichopo kwenye mchoro huanza

Ambapo hatua zake ni hizi

1.BAADA ya kumaliza zile hatua za mwanzo juu, mjenzi/contractor huanza kazi ya ujenzi

Ambapo huanza kwa kutafuta level ya eneo

Then anahamishia vipimo vya msingi kwenye ardhi yaani setting out, ambapo hapo atakuwa na mambo, kamba, chokaa, misumari, nyundo panga n.k

Hatua inayofuata ni kuchimba msingi kulingana na setting out na mchoro, ikumbukwe kuwa kwa standard ya ujenzi tuliyoadapt kwenye ujenzi Tanzania ni British standard as assumed ardhi kubwa ya kitanzania ukianzia na urefu wa 1.5m Mara nyingi ardhi ngumu utakuwa umeikuta, na ndio maana karibu mchoro mingi ya structural urefu wa shimo unakuwa 1.8 yaani 0.3 m kwa ajili ya working space..

So kwa assumption nachukulia michoro mingi niliyotumia Mimi ambapo pad foundation huwa 1.5m deep

BAADA ya mashimo ya msingi kuchimba kinachofuata huwa ni maandalizi ya kitanda cha kitako, yaani foundation bed ambapo hutengenezwa kazege karatio ndongo (blinding) km 1:4:8 suggestions ni iwe grade 15 unamwaga chini kwenye shimo kwa thickness isiyozidi 2.5mm, hii ni kwa ajili ya kupokea kitako, kuondoa vumbi na uchafu pia kutengeneza bond na ardhi.

Then inatengenezwa formwork ya base, na maandalizi ya nondo I.e chuma za base pia huandaliwa kwa kufuata structural drawings, lakini mchoro ya structural na architectural yote inatakiwa isomwe pamoja
Formwork ya base huwa inahitaji marine moja, 4×2 PCs 4 misumari nchi 2½ na 3 nusu kilo kila moja..

Na chuma Mara nyingi hufungwa kwa spacing isiyozidi 20cm kati ya nondo moja na nondo nyingine ambayo hii huhitaji nondo mbili kama itasukwa top na bottom ikisukwa mlalo mmoja ni nondo moja huhitajika (hesabu ni kwa base moja/shimo moja)

Shukrani za dhati toka kwa mdau wetu 0659299753 Mayuma chams

No comments :