Social Icons


RANGI ZA NYUMBA ZINAZOROCK KWA SASA

Ukuaji wa teknolojia umeongeza kwa kasi mabadiliko katika ujenzi wa nyumba zetu.miaka ya nyuma wengi walipaka rangi cream au nyeupe kwa ndani tofauti na sikuhz ambapo rangi huchanganywa kwa teknolojia ya kisasa ya kutumia compyuta na kupelekea kuongeza uwigo mpana wa uchaguzi wa rangi za kupaka ndani na nje ya nyumba zetu.
Muhimu kuzingatia ni kuwa rangi hizi znazoshine kwasana mfano orange, zinapendeza kuwekwa kwa ukuta mmoja tu kwa ndani na kwingne zinabaki rangi zisizo na kelele yaani zilizotulia.Zaid kwenye vyumba vya watoto wa kiume wengi hupendelea blue wakati kwa wakike pink,purple na orange au green hupendeza zaid.
Kama ilivyo ada tunakupa mifano kwa picha na itakusaidia kukupa maamuzi pale utakapohitaji kununua rangi za nyumva yako.Zaidi sikuhiz rangi hata gypsum zinapendeza ukiweka tofauti na nyeupe kama wengi walivyozoea.(picha ya rangi za gypsum toka kwa mdau wangu wa ujenzi zone)

UJENZI ZONE METAL WORKS NOW OPEN AT MWENGE

Tunapokea oda za madirisha na milango, mageti,balcon,vitanda na kazi zote za grill.karibuni sana ofisi zetu zipo goba mbezijuu .kwa uliye Dsm na vitongoji vyake tunakupimia, tunakupa design uchague kisha tunakupa quotation ukiafiki kazi inaanza kwa muda mfupi.karibuni sana namba za watsap ni 0717060776

FINISHING NZURI NDIO PAMBO LA NYUMBA..

Hauhitaji maua mengi,au rangi kali na nyingi kuipendezesha nyumba.Finishing nzuri ndio pambo la uhakika kwa nyumba yako.Hatua ya finishing inahusisha uwekaji wa vitu mbali mbali baada ya phase One kukamilika yaani hatua ya jengo.
Uwekaji plasta,skimming,floor,tiles,ceiling design mfano gypsum boards,fittings ya vitu mbalimbali mfano jiko,makabati,taa,mabafu,vyoo,madirisha ya vioo ,na milango hata rangi ya nje na ndani ndio huleta sura kamili ya nyumba zetu.Leo tutatizama vitu muhimu kuzingatia kwa finishing ya nje ya nyumba.mpangilio mzuri wa rangi zinazopakwa kwa nguzo na ukuta nazo huzidisha mvuto,Muhimu sana rangi zisizidi mbili kwa nje na uzingatie rangi ya paa lako na mwenendo mzima wa rangi za nyumba ziwe zinaendana.Kama ilivyo ada yetu tunakupa ideas zaidi kupitia picha.(pichani utaona nyumba zinavyovutia nje na hii yote ni sababu ya finishing iliyotulia toka kwa mafundi waliotuliza akili na kuzijua kazi zao.kwa kazi hizi waone ALCANE wana page yao facebook,kazi za tiles muone fundi0752128280,urembo wa nguzo muone fundi0714 532905,skimming na rangi muone 0687789024)

SAFIRI NA UJENZI ZONE ..JIONEE UJENZI WA NYUMBA ZA WENZETU

Karibu katika segment hii mpya kwa Ujenzi zone blog.leo tumesafiri mpaka pande za Africa kusini kujionea nyumba za wenzetu. Tutawasafirisha kwenda sehem mbalimbali kuona wenzetu wanajenga kwa style za namna gani.Enjoy with us,uzidi kufurahia ideas mbali mbali zihusuzo ujenzi wa makazi yetu.

SHELVES IDEAS..

Katika upambaji wa nyumba na uhifadhi wa vitu muhimu kama vitabu,vinyago,na maua tunahitaji shelfu.Inapendeza   zikiwa wazi kuruhusu muonekano wa vinavyowekwa na pia ni rahisi kuzisafisha zikiwa wazi.
leo Ujenzi zone itashea nanyi ideas mbalimbali za namna ya uwekaji shelves.Wengi huzitengeneza au kuzinunua readymade na kuzifunga ukutani kwa kudrill na kufunga na screw.Zoezi hufanyika hasa kipindi cha finishing.
Karibu ujifunze kwa picha na ukaribishe wengine wajifunze kwa blog yetu.

PAZIA PLAIN COLOURS Vs PAZIA LA MAUA"IPI INAROCK?

Pazia ni kati ya vigezo muhimu vya kuzingatia kwenye kuongeza unadhifu wa nyumba zetu.
Nmekutana na nyumba zenye mapazia aina mbili kwa vigezo vya rangi. Kuna  mapazia yenye rangi moja yaani plain colour,na mengine yenye michirizi,maua  au mistari. Kiukweli nimekuwa na wakati mgumu kuchagua pazia lipi linapendezesha nyumba zetu zaidi.
  Nafahamu fika choice ya vitu kama hivi huwa subjective sababu mi maweza penda plain wewe ukapenda maua ila kuna zile general ideas,Iwapo mtu ataniomba ushauri leo achague aina gani.Muhimu kuzingatia ni kuchagua rangi ya pazia zinazoendana na rangi ya nyumba yako hasa ya ndani.(Pichani ni picha za mapazia plain na maua,je chaguo lako liko wapi?)

GYPSUM LIGHT

Tofauti na miaka ya nyuma ambapo ceiling board zilitumika zaidi ,miaka ya sasa gypsum board imependwa mno. Sababu ya umaridadi wake hasa zinapopakwa rangi inashika vizuri na pia zikiwekwa taa zile zinazozama ndani huvutia sana kama zinavyoonekana pichani.Wengi huziita gypsum light.Bei yake ni nafuu kwa mtanzania wa kawaida kumudu ,wengine hupendelea nyingi sana na wengine hupenda chache.

WASHROOM IDEAS(BLACK AND WHITE TILES ROCKS)

Nyumba bora ni pamoja na uwepo wa bafu na choo cha kisasa,kadiri miaka inavyosogea na ubunifu wa vitu hivi unatokea zaid na zaidi.kuna mabafu ya kusimama na hata ya kukaa kadiri ya chaguo lako.
Jenga ujengavyo,ila kama haujajenga choo(toilet)ni kazi bure.Starehe ya mwanadamu iko pale!Yatupasa kujenga system nzuri na imara za utoaji maji taka,halikadhalika vyumba vya  kuogea  na chumba kitakachowekwa toilet sink vinafaa viwe vikubwa na madirisha yawe makubwa kuruhusu mzunguko wa hewa.matumizi ya tiles iwe ukuta wote au nusu ukuta na chini kwa floor vimeboresha utunzaji wa mazingira ya vyoo vyetu na mabafu.
Usafi wa vyoo na mabafu ni muhimu uzingatie kila dakika aingiapo mtu kupatumia akimaliza asafishe ili mwingine au yeye mwenyewe akirudi akute pako safi.
Leo nafurahi kushea nanyi toilet ya mdau wangu,ameweka tiles nzuri black and white chini na ukutani na hakika panavutia na pasafi.hii sio google, wadau wanafanya kweli hakika watanzania tunaweza.zaidi utaona picha ya bafu la kisasa haihitaji kuyasukuma maji kwa fagio wala brashi,zinaitwa shower cabin kwa lugha za wenzetu.mwishoni utaona mabafu ya wenzetu(tiles nyeusi zinafaa bafuni) na mwishoni utaona bafu la crazy colour.

TV WALL NDIO HABARI YA MUJINI

Karibu katika blog yetu ya kitanzania upate mawazo maridadi toka kwa wazoefu wa masuala ya ujenzi na nyumba.
Leo Ujenzi zone itashea nanyi uzoefu jinsi ya kuandaa ukuta mmoja sebuleni kwako kwa maandalizi ya kuweka tv.Maandalizi haya ni moja ya unadhifu kwa nyumba zetu.wengine hujengea nguzo na kuzidecorate wakati ujenzi unaendelea,wengine hupainua mfano wa stage ndogo na wengine huandaa  wakati wa finishing hatua zile  za mwisho baada ya rangi.
Ipambe tv wall yako kwa wall paper,tiles au tanga stone ili kuleta utofauti na kuta zingine katika sebule yako. Hakikisha unaweka socket za umeme na bomba za kupitisha nyaya za antena kabla hujaanza kuremba wall yako kwa mawe,tiles nk.hii itasaidia kuifanya wall yako smart kwani haitakuwa na nyaya zinazoning'inia(maelezo na picha kwa hisani ya mdau wangu wa ujenzi zone Mr.Abeid Gallus Abeid. Karibu sana mdau wowote kushea uzoefu nasi kwa watsapp 0717 060776)

GLASS BLOCKS KWA MVUTO WA NYUMBA

Ni aina ya vitofali vidogo kwa size vilivyotengenezwa na kioo kizito pande zote.zipo madukani na wengi hununua  kwajili ya finishing ya nyumba zetu.Wengi hupendelea kuweka kwenye ngazi sababu zinaingiza mwanga lakini hazipitishi hewa na walio nje hawawezi ona ndani.Zinakuja na rangi tofauti hasa blue,kijani au rangi ya kioo plain.kwa kifahamu zaidi pitia picha zifuatazo(0767287708fundi wa kuweka glass bloks)