Social Icons


TIPS MUHIMU KUHUSU FREM ZA BIASHARA MAENEO YA MAKAZI..

Mada hii imetumwa na mdau mwenzetu ambaye amekuwa akitushirikisha mengi yenye faida kwetu..

Ni kuhusu ujenzi wa fremu za biashara katika maeneo tunayojenga nyumba za kuishi.

Ni ukweli usiopingika kuwa wenye nyumba hujenga pia fremu ili kujiongezea kipato kutokana na kodi au kusogeza huduma muhimu katika eneo husika hasa kwa wanaoamua kujenga nje sana ya mji ambako ndio rahisi kupata plots kubwa.

Ushauri wangu kwa wadau wanaoplan kujenga fremu za biashara kwenye nyumba zao ni kama ifuatavyo:

1. Mandhari ya fremu ifanane na nyumba kubwa (kwa rangi, upauaji, etc)

2. Kama ni fremu zaidi ya moja, basi ni vema kujitahidi kuweka mita ya umeme (luku) kwa kila fremu ili kuepusha usumbufu kwa wapangaji

3. Ni muhimu sana kujenga choo kwa matumizi ya hao watakaokodi fremu zako ili wasisumbuke hapi mtaani

4. Landscaping au upambaji wa sehemu ya biashara kama kuweka maua ni muhimu sana siku hizi kwani ni sehemu pia ya mvuto kwa watakaohitaji bidhaa toka kwa hao wapangaji wako

5. Kama plot yako ni kubwa, jitahidi fremu zikae mbali kiasi kutoka kwenye nyumba yako ili kuepuka usumbufu wa aina yoyote kama vile miziki mikubwa toka kwa waliopanga kwenye fremu zako

6. Pia ikiwezekana ni muhimu sana kuweka mfumo wa maji wenye uhakika kwa ajili ya matumizi ya choo na hata kwa mpangaji atakayetaka fremu kwa ajili ya biashara kama saluni au barber shop (kinyozi).

7. Mwisho ni sehemu ya parking ya magari kulingana na idadi ya fremu zako.

TUNASHUKURU SANA MDAU KWA MADA HII..UJENZI ZONE INAKUPONGEZA KWA KUJENGA FREM HIZI ZA KISASA,PIA HII NI  HUDUMA KWA JAMII NA INASAIDIA SANA KUSOGEZA HUDUMA MUHIMU KAMA DUKA LA VYAKULA,SALUNI,PHAMACY N.K JIRANI NA MAKAZI.

No comments :