Social Icons


BALCON DESIGNS (BEFORE AND AFTER)

Imekuwa kawaida nyumba zetu kuwa na baraza mbili ya mbele na ya nyuma.Maranying hii ya mbele ndio hubeba sura ya nyumba zetu.Hivyo inapendeza tukiipa muonekano mzuri,wengine hupendelea kuweka uzio wa maua ya zege,wengine huweka uzio wa maua ya chuma,na wengine hupendelea aluminium pipes kana zinavyoonekana pichani..(Asante madam admn.kushea nasi balcon ya nyumba yako before and after..)
Kuna aina ya viti vizuri maalumu kwajili ya barazani.wengine huweka vya plastic matirio,wengine huweka vya mbao,halikadhalika kuna matirio ya aina tofauti jamii ya mianzi ambayo hupendeza na kuvutia iwekwapo barazani.
Muhimu ni kuzijali baraza zetu kwa kuzipa nafasi ya kutosha, kwa taa nzuri,rangi nzuri,pia tiles nzuri na kuzijali muda wote kwani ndio ilipo sura ya nyumba zetu.Muda mwingine baraza hutumika sawa na zilivyo sebule kwa nyakati tofauti.(0786 808707 kwa kazi za metal balcon)

HYDRAFORM BLOCKS NDIO HABARI YA UJENZI WA KISASA

ASSET YANGU Kampuni ya kitanzania yenye nia ya kuona wateja wake mnamiliki....haikupi tu habari za  wapi ilipo nyumba, shamba au kiwanja..bali inakupa mwelekeo jinsi gani utajenga kwa gharama nafuu na ubora wa hali ya juu.
SASA TUNAFYATUA NA KUUZA HYDRAFORM BLOCKS BEI NI SHILING 600 KWA BLOCK 1,NA 700KWA BLOCK MOJA PAMOJA NA UPAKIZI.
UKIHITAJI TUFYATULIE KWAKO BEI NI ILE ILE 600,MUHIMU MAJI NA ENEO LIWE ZURI NA NAFASI YA KUTOSHA.
Site iko  BAHARI BEACH..ZAIDI UKIHITAJI MAFUNDI WATAALAMU WA KUZIJENGEA TUTAKULINK NAO.
0713 551328.karibu

SALAMU ZA UPENDO KWA WADAU WOTE WA UZ BLOG

Administrator wa blog ninayo furaha kuwakaribisha wote wenye maswali,maoni,na wenye kutaka kushea nasi chochote kuhusucho ujenzi zone blog..tuwasliane kwa watsapp namba 0717060776 na 0786808707.
Kutokana na sababu za kiufundi admn amekuwa anashindwa kujibu maswali yenu kwenye chatroll ila hivi karibuni tutakuwa pamoja.
Admin anajihusisha na kazi za grill  kuanzia madirisha,mageti,na fenicha zote za chuma. Tangazo letu linazo namba za admin hivyo utanipata moja kwa moja.KARIBUNI NA ASANTENI KWA USHIRIKI MZURI,KARIBU FACEBOOK UJENZI ZONE GROUP INAKUWA NA MADA ZA UELEWA KILA SIKU KUHUSU UJENZI

SITTING ROOMS ZINAZOROCK...

Blog yako ya Ujenzi zone leo itakupa somo kuhusu mionekano tofauti ya sebule zetu zinavyotakiwa kuwa' na hii yote ni kukuongezea ideas ambazo ukizifanyia kazi utaifanya sebule yako iwe paradiso ndogo na kukuvuta uwahi nyumbani muda wote.
Muhimu kabisa kwa tunaoanza ujenzi tuzingatie kuzipa sebule zetu nafasi ya upendeleo ili ziwe na hewa na mwanga wa kutosha kuhimili mzunguko wa watu.
Pili,tuzingatie urembo wa ceiling kama gypsum basi iwe na muundo tofauti kidogo na vyumbani ilimradi mvuto uongezeke.
Wakati ujenzi unaendelea waweza dizain nguzo fulani au steps za kushuka au kupanda plus tv wall ilimradi pawe na mvuto wa kile unachokipendelea,wengine hujengea glass blocks kwa ndani,pia kabati la kuweka tv ni vyema likadzainiwa likae wapi mapema(showcase).
Baada ya ujenzi zingatia taa nzuri,rangi tofauti kwa ukuta mmoja, picha nzuri za ukutani,shelves za kisasa nazo huongeza umaridadi,makochi mazuri,capet nzuri na coffee table nzuri.
Hauhitaji makorokoro mengi sana kuipendezesha sebule yako ni kuwa na usefull staffs chache na zenye muonekano mzuri.
Wall pepa zikidizainiwa vizuri especially kwa kuta moja mfano tv wall nazo huvutia sana.
Picha za ukutani ni vyema ikawa moja kubwa na nzuri na sio zijae kuta pande zote za sebule,nyingine weka kwa corido na kadhalika,maana zikizidi mbili inakuwa sio tulivu.
Jionee kwa picha na utapata wazo..(Specially thanks kwa mdau wetu Abed Gallus Abed kushea nasi  baadhi ya picha za sebule).HAUJACHELEWA KUSHEA NASI PICHA ZA VITU MBALIMBALI VIHUSUVYO UJENZI NA USIACHE KUTANGAZA NASI 0717060776 WATSAP

FROM NOTHING TO SOMETHING...

Safari hii ni ndefu sana na bila shaka ina headache za hali ya juu ambazo huwa hazihesabiwi kabisa katika utaratibu wowote wa gharama ya nyumba.
Ifike pahala tuwaheshimu wenye nyumba na kuzijali nyumba zao katika mazingira yoyote tunayojikuta tunaishi katika nyumba hizo.Uwe ni mpangaji,au mfanyakazi bado unawajibishwa kutunza nyumba hizi ili zidumu zaidi.
Imekuwa ni desturi kuona baba mwenye nyumba au mama mwenye nyumba ni mkorofi na adui ila utakapojikuta umeanza safari hii ndio utagundua kwanini na wao walipanga masharti mengi na hata walikereka kuona mwanao anapochora ukuta na mkaa au na msumari.
Muhimu ni kuwa tuheshimu, tutunze,na tuthamini jitihada za wenye nyumba kwani safari hii sio pesa tu ndio huiongoza bali muda na kujitoa kwa hali juu tena kwa wenye hofu ya mungu tunasema safari hii ni kwa neema zake mungu ndio huifanikisha.
Nawatakia safari njema mnaoanza ujenzi,mlio hatua za katikati,na mliomaliza nawapongeza sana munayo haki  ya kuzisimamia nyumba zenu kwa umakini wa hali ya juu ili zizidi kudumu.
HESHIMA KWA BABA NA MAMA MWENYE NYUMBA.Mujini wanasema hakuna baba  mwenye gari ni baba mwenye nyumba tuu.(shukrani kwa wadau wote wa ujenzi zone kufanikisha uwepo wa picha hizi)